HIZI HAPA AHADI ZA DKT. SAMIA  AMEHIDI GEITA VIJIJINI , AIGUSA SEKTA YA AFYA HUDUMA ZAIDI ZA MATIBABU NA VIPIMO 

GEITA

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kusogeza huduma za afya karibu zaidi na Wananchi wa Geita Vijijini Mkoani Geita pamoja na ununuzi wa vifaatiba na vipimo vya kisasa ili kuondoa adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama kubwa kufuata matibabu. 

Dkt. Samia ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2025 mbele ya maelfu ya wananchi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM, wakati wa muendelezo wa Kampeni zake Mkoani Geita kwenye Kata ya Nyawilimilwa akiahidi kuongeza Vituo vya afya na Zahanati katika maeneo ambayo bado hayajapata huduma hizo kwa wananchi.

 Dkt. Samia kadhalika ameeleza kuhusu ununuzi wa mashine za vipimo za kisasa ikiwemo mashine za Xray na CT scan ili kuhakikisha huduma zote muhimu za afya na matibabu zinapatikana ndani ya Mkoa huo.

Aidha  amewataka wananchi wa Geita Vijijini pia kujiandaa kikamilifu na ujio wa bima ya afya kwa wote, akisisitiza kuwa ndani ya siku mia moja za kwanza madarakani ataanza majaribio ya bima hiyo ya afya, suala ambalo litaondoa adha ya wengi kushindwa kumudu gharama za matibabu pamoja na kuondoa kero ya kuzuiwa kwa miili ya watu pale wanapofariki wakiwa na madeni ya matibabu kwenye Hospitali.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000