MATUKIO PICHANI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Nchi mbalimbali mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA nje ya ukumbiwa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia ambao unatoa mikopo nafuu na misaadakwa nchi zinazoendelea.

PICHA YA CHINI NI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi pamoja na Wageni mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia ambao unatoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.




Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000

