Mjema ageuza idara ya uenezi kuwa ya familia yake na mumewe
Wakati idara ya uenezi ya CCM ikikumbwa na kila aina ya kashfa za kufeli kufanya majukumu yake na mgogoro usioisha kati ya mwenezi na katibu wake mkuu Chongolo kuna shutuma zimeibuka kumhusu katibu mwenezi Sophia Mjema kuwa kageuza ofisi ya chama kuwa suala la kifamilia.
Imefika mahali mume wa katibu mwenezi bwana Shaaban Mwanga anajitambulisha kama Mr Mwenezi kwa wadau wa siasa na biashara anapokuwa anatumwa na mkewe kwenye majukumu yake ya kupokea na kukushanya rushwa. Tunajiuliza je? Nafasi hii inatambulika ndani ya katiba ya CCM? Mume wa mwenezi ni sehemu ya uongozi wa CCM?
Kilichopo sasa CCM ni viongozi wa juu akiwemo makamu , katibu mkuu na mwenezi ni kujitafutia utajiri binafsi kupitia mwamvuli wa CCM ndiyo maana chama kinakwenda tu kwa nguvu za upepo na viongozi wanapishindana kupokea rushwa na kukamua wafanyabiashara.
Katibu Mkuu Chongolo yeye kazi yake ni kukusanya hela kwa wadau na wafanyabiashara kwa kigezo cha kusaidia chama lakini kinachofanyika ni kwa kusimamisha maghorofa kila kona na kununua magari ya kifahali.
Chongolo anawezaje kuwa na majumba zaidi ya 40 Dar Es Salaam? Anapata wapi huo uwezo? Haya mambo aliyaanza kuyafanya toka akiwa Kinondoni na hajawahi kuacha ufisadi anaoufanya na sasa anatumia kiti cha ukatibu mkuu kujilimbikizia mali kwa kiwango cha kifisadi sana.
Chanzo chetu kimetuambia kuwa anapoambiwa na watu wake wa karibu juu ya mwenendo wake na kumtaka kuchukua tahadhari kwa kuwa mambo haya hayatamfurahisha mwenyekiti wa chama akajibu kuwa “mwenyekiti ana madaraka lakini hana watu , sisi tuna watu” kauli hii ni ya kifedhuli na dharau sana kwa mwenyekiti wake na kwa kweli kama hatachukuliwa hatua huyu ana hatari sana ya kuja kukiletea chama hiki majeraha makubwa sana mnele ya safari. Huyu atakuwa katibu mkuu wa hovyo sana aliungana na Mukama na Makamba ambaye mpaka sasa ndiye mwenye rekodi ya kuwa katibu nkuu wa hivyo kukiko wote.
Mr Mwenezi (Shabani Mwanga) kupitia mkewe wanajipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa wadau wa siasa na wafanyabiashara na tunaambiwa zinapitishwa kwenye akaunti za vyuo vyao vya City Colleges kama njia ya kujificha na ufisadi huo.
Hata matukio ya Mr Mwenezi kufadhili mashindano mbalimbali na shughuli za kijamii ni utapeli tu wa kufunika uozo na ufisadi wao.
Inakuwaje majukumu na kazi zinazofanywa na mwenezi zinalipwa na City Colleges kupitia mumewe? Au City Colleges ni vyuo vya CCM? Au City Colleges imekuwa ni idara ya fedha ya CCM pale Lumumba? Kama siyo inakuwaje mume wa mwenezi analipia shughuli anazofanya mkewe kama mwenezi wa chama?
CCM inapoteza hadhi yake kwa kuwa na viongozi wa aina ya Chongolo na Mjema na haya mambo ndiyo yakiyofanya bwana yule kutaka ku reform CCM kwa kuwa imeshikwa na majizi.
Endeleeni kumkumbatia Mjema na Chongolo lakini matokeo yake mtayaona hivi karibuni. Watanzania siyo wajinga kama mnavyodhania.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000

