RAIS DKT MWINYI ALIPOKUTANA NA KUNDI LA VIJANA WA UVCCM

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema wakati umefika kwa Vijana kukataa siasa za Ubaguzi na Chuki.
Amesema Tangu awamu ya nane iingie madarakani imesimamia
Umoja,Amani na Mshikamano na kuwataka Vijana kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda Uchaguzi.
Rais Dkt, Mwinyi amesema hatima ya Taifa imo Mikononi mwa Vijana kwa kuwa zaidi ya asilimia 65 ya Wananchi ni Vijana na kuwasisitiza kulinda Amani ya Nchi kwa nguvu zao zote.
Ameeleza kuwa vijana Wamethibitisha kuwa wanaweza kufanya vizuri wanapokabidhiwa Dhamana na tayari amelithibitisha jambo hilo.
Amewahakikishia Vijana kuwa uongozi Ujao baada ya CCM kushinda Uchaguzi nafasi nyingi za Uteuzi zitakuwa kwa Vijana na kukiri kuwa Vijana na Wanawakee aliowateua Awamu iliopita katika nafasi mbali mbali Hawakumuangusha .

Ameahidi Ajira kwa Vijana wengi zaidi katika ajira za Serikali na kwamba Serikali inajipanga kuleta Wawekezaji wengi katika sekta ya Viwanda kuja kuwekeza Zanzibar ili kutoa fursa kwaVijana.
Raiis Dkt, Mwinyi amesema baada ya kufanikiwa katika sekta ya Elimu ,Afya na nyenginezo sasa nguvu zote zinaelekezwa kwa Ajirra kwa vijana ikiwemo kuwapatia Mikopo isio na riba ili wajiajiri wenyewe na mafunzo ya stadi mbalimbali.
Raiis Dkt, Mwinyi amesema Chama hicho kina Uhakika wa Ushindi katika Uchaguzi kwa kuwa na Jumuiya ya Vijana na ya UWT pamoja na Wazazi ambazo zinafanya kazi nzuri ya kutafuta Kura.
Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Makundi ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Pemba ikiwa ni muendele,o wa Kampeni zake kisiwani humo hafla iliofanyika ukumbi wa Mikutano Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Rais Dkt Mwinyi amewahakikishia Vijana kuwa Serika ijayo inakusudia kutoa ajira zqidi na mkazo wa kuwaajiri Vijana wa Makundi ya Hamasa yalioshiriki Uchaguzi wa Mwaka huu na kuiagiza UVCCM na Watendaji wa Chama Kuandaa majina ya Vijana hao mapema.
Naibu Katibu Mkuu wa CCm Zanzibar Dkt,Muhammed Said Dimwa amesema UVCCM ni nguvu ya Mabadiliko ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuwaagiza Vijana kufanyakazi muhimu ya kusaka kura za Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ili kipate Ushindi wa Kishindo tarehe 29 Oktoba 2025.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000