RAIS MWINYI NA WAKANDARASI WA SEKTA YA UJENZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameizindua Jumuiya ya Wakandarasi wa Sekta ya Ujenzi Zanzibar na kuahidi Serikali kuendelea kushirikiana na Wadau wote wa Sekta hiyo kutokana na Umuhimu wake katika Mipango ya Serikali.
Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 11 Oktoba 2025 wakati akiizindua Jumuiya hiyo hafla iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip ,Uwanja wa Ndege Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amefahamisha kuwa katika miaka ya karibuni Serikali imefanya Mageuzi Makubwa katika Sekta ya Ujenzi kwa kujenga Miundombinu mbalimbali ikiwemo Barabara, Skuli na Hosptali hivyo kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo kutatoa fursa ya Ushrikiano, Mijadala na Taaluma kwa Serikali katika kutekeleza Miradi ya Ujenzi.

Rais Dkt, Mwinyi ameipongeza hatua ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo
alioielezea kuwa ni Chombo muhimu cha kuwasilisha Changamoto,Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali itakayoiimarisha Sekta ya Ujenzi hapa Nchini.
Ameeleza kuwa kwa Sekta ya Ujenzi Zanzibar imefungua Historia mpya ya kuleta Ushirikiano wa Wadau wa ujenzi na Serikali kufanya Kazi kwa pamoja kwa ajili ya kuchochea Maendeleo ya sekta ya Ujenzi
Rais Dkt, Mwinyi amewahakikishia Wadau hao kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Jumuiya hiyo ili iendelee kutoa mchango wake katika kuimarisha sekta hiyo na Ukuaji wa sekta nyengine za kiuchumi hapa nchini.
Aidha ameahidi Serikali itazifanyia Kazi Changamoto zote ziliomo katika sekta ya Ujenzi na zile zitakazojitokeza ili sekta hiyo iendelee kutoa Mchango wake kwa Maendeleo ya Nchi.
Kuhusiana na Suala la kukosa Mitaji kwa Wadau ameiagiza Wizara ya Ujenzi pamoja na Bodi ya Wakandarasi kuwaunganisha wadau na Taasisi za Kifedha ili kupata mikopo pamoja na kuangalia Uwezekano wa kuandaa Mifuko kwa ajili kuwasaidia Wadau wa sekta hiyo.
Rais Dkt, Mwinyi amewasisitiza wadau hao kuwa na Umoja ,Mshikamano na kuepuka Migogoro isio na tija kwani Wana wajibu wa kushirikiana kwa ajili ya Maendeleo ya Sekta ya Ujenzi .
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzì

Dkt, Khalid Salum Mohammed amesema kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ni Maono ya ya Rais Dkt, Mwinyi yanayochochea Uendelezwaji wa Miradi ya Kimkakati katika sekta mbalimbali hapa nchini
Akiwasilisha Taarifa ya Wadau wa sekta ya Ujenzi Zanzibar Mwenyekiti wa ZCSA
Nd, Said Omar Fakih ameeleza kuwa lengo kuu ni Kuwaunganisha Wadau wa Sekta ya Ujenzi kuwa na Sauti moja, kupata fursa za kazi za Ujenzi, Mafunzo na Mitaji kwa Wadau.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakandarasi na Wadau Shirikishi wa Ujenzi Tanzania (TUCASA) Nd,Samuel Marwa amefahamisha kuwa wakati Umefika wa Wakandarasi Wazalendo kuijenga nchi yao wenyewe badala ya Kutegemea Wageni na kusisitiza Ushirikaino baina ya TUCASA na ZCSA.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000